Clara Luvanga Staa Yanga hadi bingwa kwa Ronaldo

Clara Luvanga Staa Yanga hadi bingwa kwa Ronaldo


Mwanadada Clara Luvanga anazidi kuki-washa nchini Saudi Arabia ambako mwishoni mwa wiki iliyopita alifanya makubwa wakati timu yake ya Al Nassr ikitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya wanawake kwa kuifunga Al Hilal 4-2 na kufikisha pointi 31 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kwenye mechi nne zilizosalia.


Timu hiyo imebeba ubingwa kwa mara ya pili mfululizo na huu ni ubingwa wa kwanza kwa staa huyo kwenye maisha yake ya soka baada ya awali kushindwa kuchukua akiwa na Yanga Princess kabla ya kwenda Saudia.


Amekuwa na msaada wa kutosha kwenye kikosi hicho na tangu ajiunge na waarabu hao amefunga mabao 11, likiwamo moja na asisti mbili alizozitoa katika ushindi wa 4-2 dhidi ya Al Hilal katika mechi iliyowapa ubingwa huo Ijumaa iliyopita Machi


Timu ya Al Nassr (W) ni klabu moja na timu ya Al Nassr ya wanaume anayochezea supas-taa wa dunia, Cristiano Ronaldo, ambaye ana-tajwa kuwa alichangia timu hiyo ya wanawake kutwaa ubingwa wake wa kwanza katika historia msimu uliopita pale alipoibuka mazoezi-ni kwa kinadada hao zikiwa zimesalia mechi mbili msimu kwisha na akazungumza na wachezaji kuwapa hamasa ya kuwataka wapambane hadi wapate ubingwa.


Baadaye Ronaldo akaposti picha za ziara yake hiyo kwenye kambi ya mazoezi ya timu yao ya wanawake katika akaunti zake za mitandano ya kijamii zenye wafuasi milioni 901.


NJIA ALIYOPITA Kabla ya kujiunga na Yanga Princess ambako ndipo alipata umaarufu mshambuliaji huyo alicheza Mapinduzi Queens msimu wa 2020 ilikuwa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza na kui-pandisha hadi Ligi Kuu na msimu uliofuata akajiunga na timu ya wananchi.


Akadumu Yanga kwa misimu miwili Agosti 2023 akajiunga na Dux Logrono ya Hispania alikodumu kwa miezi mitatu tu na kusajiliwa Saudia.


Dux Logrono ya Hispania ndio timu ya kwanza kucheza nje ya nchi na mechi ya kwanza ali-ingia kutokea benchini katika dakika ya 60 na alifunga bao moja timu yake ilipoondoka na ushindi wa mabao 7-0.


Hispania alisaini mkataba wa miaka miwili lakini ubora aliouonyesha kwenye kikosi hicho uliwavutia waarabu hao ambao walimfuata na kuvunja mkataba wake. Timu hiyo ilikuwa ikishiriki Ligi Daraja la Kwan-za na baada ya Clara kufunga katika mechi ya kwanza ndio ilimpa namba kwenye kikosi cha kwanza.


Kutokana na ufundi wake ikawa rahisi kuyashawishi mataifa mawili kutaka saini yake yaani timu kutoka England na Al Nassr kutoka Saudi Arabia ambayo ilimpa ofa nono zaidi.


MABAO YAKE Tangu ametua uarabuni timu yake imecheza mechi 11 na ametupia mabao 11 wastani wa kufunga bao moja katika kila mechi na anaongoza orodha ya vinara wa ufungaji. Sio ajabu kumuona akifunga mabao matamu na kiwango chake kimemfanya ashinde tuzo ya Bao Bora la Mwezi Septemba akipiga shuti la umbali mrefu na kujizolea umaarufu.


Clara ni mwamba kwelikweli katika kucheka na nyavu. Msimu wa 2022 akiwa na Yanga Princess aliweka kambani mabao 13 na haku-cheza mechi nyingi kutokana na majukumu ya kupigania taifa kwenye mashindano ya Kombe la Dunia yaliyofanyika nchini India.


Mbali na kuisaidia timu yake aliwahi kuwa mfungaji bora kwenye timu ya taifa ya vijana ya Serengeti Girls U-17 nchini India akimaliza na mabao 10 na kuisaidia timu hiyo kufuzu kucheza Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia.


KIATU Tangu acheze soka nchini, Clara hakuwahi kuchukua tuzo ya mfungaji bora wa ligi na huenda msimu huu kismati cha Kiatu cha Dhahabu kikamdondokea.


Ligi ya Saudia kila timu inacheza mechi 14 zikiwa zimesalia mechi tatu za kuamua hatma ya kubeba kiatu akitofautiana bao moja na wenzake wanaomfuatia, Ibtisam Jraidi wa Al Ahli na Sara Al Hamad wa Al Nassr wakiwa na 10 kila mmoja.


Juzi kupitia mitandao ya kijamii ya timu yake iliposti video fupi ikimuonyesha namna Clara alivyomalizia pasi ya kichwa huku ikisindikizwa na maneno yaliyosema 'Clara hakosi bao'.


MALKIA SASA Baada ya nahodha wa timu ya taifa 'Taifa Stars', Mbwana Samatta na Simon Msuva kufanya makubwa kimataifa, kwa sasa malkia wa soka ni Clara.


Wapo wachezaji wengi wa kike wanaofanya vizuri kimataifa akiwemo Aisha Masaka (BK Hacken ya Sweden), Enekia Lunyamila (East-ern Flames ya Saudia), Diana Msewa (Amed SK ya Uturuki), Julietha Singano (Juarez - Mexico) na Opah Clement (Besiktas - Uturuki).


Wote hao ni malkia wa soka kwa sasa lakini kutokana na kiwango bora na ndio straika tegemeo na anayetazamwa zaidi basi huenda akapita njia za Samatta aliyeliwakilisha vyema taifa la Tanzania.


MSIKIE MWENYEWE "Nimefurahi sana kuchukua ubingwa ilikuwa ndoto yangu siku moja na mimi nivae medali na kuisaidia timu, nimefurahi ndoto yangu ya kwanza imetimia tena nikiwa nje," alisema Clara, ambaye ndoto yake ya pili ni kutwaa Kiatu cha Dhahabu cha mfungaji bora.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.