Wakati Edo Kumwembe Akimponda Kocha Benchikha, Ahmed Ally Kamjibu Haya

 

Kocha Benchikha Vs Edo Kumwembe
 Kocha Benchikha Vs Edo Kumwembe

Wakati Edo Kumwembe Akimponda Kocha Benchikha, Ahmed Ally Kamjibu Haya

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema mara baada ya Simba kuanza kufundishwa na kocha wao mpya Benchikha, mazoezi yake yanavutia.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ahmed ameweka ujumbe huo akionesha ana hamu ya kwenda kuangalia mazoezi ya Benchikha.

“Muda ufike tuu tuende mazoezini siku hizi raha kweli kuona mazoezini yetu. Raha unayoipata kuiona Simba ya Benchikha ni kama kupokea mshahara au kuvunja kikoba.”


SOMA PIA: Ligi Bora Africa | Best Football Leagues in Africa 2023/2024


Aidha katika hatua nyingine,Mchambuzi wa soka nchini Edo Kumwembe amesema, tabia au hulka ya viongozi wa Simba na kocha wao mpya Benchikha zinafanana sio watu wa uvumilivu.

Amesema Benchikha akiona unamzingua hakawii kukuachia timu kama ilivyo kwa uongozi wa Simba, wanasifikika kwa kutimua walimu.

“Simba na Benchikha wana tabia sawa, ndio maana unaona Bechikha kashahama vilabu vingi, Raja kafundisha mara mbili sijui hivyo wana tabia sawa,” alisema Edo.


SOMA PIA: ORODHA ya Vilabu Bora Afrika 2023 (CAF Club Ranking)


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.