Ronaldo atemwa Wanasoka bora 100, Messi ndani

 

Ronaldo atemwa Wanasoka bora 100, Messi ndani

 Ronaldo atemwa Wanasoka bora 100, Messi ndani

Siriazi? Orodha ya wanasoka 100 bora duniani imetoka na utashangaa Cristiano Ronaldo hayumo. Ndiyo hivyo. Mkali huyo anayekipiga Al Nassr ya Saudi Arabia, hayumo kwenye orodha hiyo, huku Jude Bellingham akitajwa kwenye namba mbili.


Wakati mwaka 2023 ukielekea ukingoni, mtandao wa FourFourTwo umetoa orodha ya wanasoka walioonyesha ubora mkubwa kwa kuanzia mwaka jana hadi sasa na kwenye orodha ya wakali 100, supastaa Ronaldo hayumo. Mastaa kama Bruno Fernandes, Gabriel Martinelli, James Maddison, Virgil van Dijk na Son Heungmin wamejumuishwa kwenye 100 bora, lakini Ronaldo mwenye Ballon d’Or tano amekosekana.


Hata hivyo, mpinzani wake wa miaka mingi, Lionel Messi bado yumo kwenye orodha licha ya kushindwa kuwamo kwenye Tano Bora. Messi, aliweka rekodi ya kushinda Ballon d’Or yake ya nane, ametajwa kushika namba sita kwenye orodha hiyo ya FourFourTwo ya kuhusu wanasoka 100 bora duniani.


Messi, 36, aliisaidia Argentina kushinda Kombe la Dunia mwishoni mwa mwaka jana na kushinda Golden Ball na Juni mwaka huu alijiunga na Inter Miami alipoachana na PSG kama mchezaji huru, ambako amefunga mabao 11 na kuasisti mara tan

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.