Pamoja na Kupigwa Zengwe Simba Hivi Ndivyo John Bocco Alivyoendelea Kupigilia Msumari Rekodi yake ya Magoli Ligi Kuu

Pamoja na Kupigwa Zengwe Simba Hivi Ndivyo John Bocco Alivyoendelea Kupigilia Msumari Rekodi yake ya Magoli Ligi Kuu


Katika mchezo wa juzi dhidi ya Kagera Sugar, Nahonda wa Simba John Bocco aliingia dakika ya 80 na kufunga goli la mwisho kwa timu yake katika dakika ya 90 katika mchezo ulioisha kwa Simba kuibuka na ushindi wa magoli 3-0.

Hilo lilikuwa bao la pili kwa Bocco msimu huu, lakini ni la 154 likimfanya awe Mfungaji Bora wa muda wote wa Ligi Kuu Bara akifunga mfululizo katika misimu 16 tofauti akiwa na timu za Azam FC na Simba, akimpiku mkongwe Mohmmed Hussein ‘Mmachinga’ aliyeifunga mabao 153 katika misimu 13 mfululizo.

Bao hilo lilikuwa la 70 kwa nahodha huyo katika Ligi Kuu tangu ajiunge na Simba 2017 ikiwa huu ni msimu wake wa saba na ukichanganya na yale 84 aliyofunga katika misimu tisa aliyoichezea Azam imemfanya mwamba huyo kufunika na kuwapa kazi wachezaji chipukizi kuipiku rekodi hiyo mpya aliyoiweka.

Rekodi ya Bocco ya kufunga katika misimu 16 mfululizo ilianza alipoipandisha daraja Azam katika Ligi Kuu 2007 na kuanza kuichezea ligi hiyo msimu wa 2008-2009 alipofunga bao moja kabla ya kutumia misimu 15 mfululizo iliyofuata na kuifukuzia rekodi ya Mmachinga aliyoiweka kati ya 1993 hadi 2005 alipostaafu baada ya kuzitumikia klabu za Bandari Mtwara, Yanga, Simba, Mmbanga FC na Twiga Sports

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.