Taarifa za kuaminika ni kuwa mchambuzi wa video (video analyst) wa Klabu ya Yanga, Khalil Ben Youssef alishawasili nchini Algeria wiki mbili zilizopita tayari kwa kuisoma klabu ya CR Belouizdad.
CR Belouizdad ni wapinzani wa Yanga kwenye hatua ya makundi klabu bingwa Afrika, ambapo CR Belouizdad atacheza mechi zake mbili hivi karibuni kabla ya kucheza na Yanga kwenye CAFCL.
Khalil Ben Youssef anaisoma CR Belouizdad kiufundi zaidi kwa kimfumo na kimuundo na ripoti itarudi mapema kwa Master Miguel Gamondi.