Mbwana Samatta Awatambia Wanigera Kuwania Tiket ya Kombe la Dunia

 

Mbwana Samatta Awatambia Wanigera Kuwania Tiket ya Kombe la Dunia

Nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wameweka wazi kuwa watapambana kupata matokeo kwenye mchezo wao dhidi ya Niger ambao ni wa kufuzu Kombe la Dunia. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Novemba 18 katika Mji wa Marrakech siku ya Jumamosi.

Miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara huo ni Simon Msuva, Novatus Dismas, Peter Banda, Aishi Manula, Dickson Job, Mbwana Samatta.

Nahodha Samatta amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu na ushindani mkubwa watakwenda kupambana kupata matokeo chanya.

Simon Msuva ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya kupambania taifa kwenye mechi zote za ushindani.

“Tupo hapa kwa ajili ya kupambania taifa a tunajua kuna ushindani mkubwa lakini tupo tayari na tutafanya vizuri,”.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.