Hili Taifa Stars Kutumia Makipa Wakaa Bench Kwenye Timu zao Limekaaje?

 

Hili Taifa Stars Kutumia Makipa Wakaa Bench Kwenye Timu zao Limekaaje?

Kwa mara nyingine juzi nilimsikia Kocha wa Stars akizungumzia kukosekana kwa muda wa kucheza (game time) wa makipa wake aliowaita kwenye klabu zao... Ana wasiwasi na hilo.


INASHTUA na KUOGOFYA kama eneo ambalo makosa yakifanyika ni 99% kuruhusu goli eti leo ndio eneo lenye shida😳🤔 Hata eneo la ushambuliaji lina shida zake ila hubebwa na kiungo! Golini akikosea!? Wayaa... Chuma ndani!


Kuna timu 11 kati ya 16 za Ligi zinatumia makipa wazawa kama makipa namba 1! Kati ya hao 10 ni Daniel Mgore pekee wa Dodoma Jiji walau ana Clean sheets 3 na kuwa mzawa mwenye hati nyingi safi kwenye Ligi Kuu.


Kuna namna kama nchi tumepoteza makipa wenye ubora na Aishi katusitiri kwa muda mrefu sana! Stars kati ya makipa 11 haijabahatika kuona kipa yoyote mwenye ubora wa kuitwa isipokuwa makipa wanne ambao wamekuwa benchi zaidi kuliko wale wanaocheza Kila siku!? TUMEKWAMA PAHALA.


Zamani kidogo walikuwepo makipa wengi wa kigeni lakini makipa wazawa walibaki kwenye ubora wao... Rejea Kagera walikuwa na Odo Nombo, Yanga na Obren Cirkovic / Yaw Berko, Azam na Vladimir Nniyonkuru lakini Stars haikuwahi kusumbuka.


Wangeumia wapi wakati Shaaban Dihile alikuwa bora!? Kaseja, Muharami Mohammed, Ivo Maunda, Benjamin Haule na Ivo Mapunda walikuwa na uwezo mkubwa na kuwa tayari. Ivo alienda St. George ya Ethiopia, Muharami alienda Angola.


Kwa sasa kwa viwango vya makipa kuna anayeweza kutakiwa na hizo timu?? Juzi niliweka video kadhaa hapa za kipa wa Mashujaa akitoka goli kama mshale na kuruhusu magoli ya ajabu ajabu dhidi ya Singida... Mara aruke kuwania krosi kabana mikono kama beki 😄 Ni aibu.


Kwa lugha rahisi ni kheri kumtumia Mkaa benchi wa Simba na Yanga kuliko first eleven ya KMC na Dodoma Jiji 🤔 Kocha akashauri hata itungwe kanuni ya kuwalinda makipa wazawa! Siafiki! Acha wacheze kwa uwezo wao na si kwa huruma ya kanuni.


Misri hawaruhusu kipa wa kigeni lakini makipa wao wana vituko kama wetu!? Hawa wanaoruka kama Samaki mkizi ama mithili ya viumbe visivyo na mikono?? Simba hawajasajili kipa wa nje kwa muda mrefu tu cos Aishi yupo


Kama wachezaji wa ndani wamepenya katikati ya wageni na kucheza na makipa wacheze kwa uwezo na si huruma!

Wasalaam!


✍️ Nazareth Upete

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.