Yanga Yapanda Viwango vya Ubora Duniani, Yaipiku Simba SC, Mamelodi

 

Yanga yapanda viwango vya ubora duniani, yaipiku Simba SC, Mamelodi


 Yanga yapanda viwango vya ubora duniani, yaipiku Simba SC, Mamelodi

Mtandao wa International Federation of Football History and Statistics (IFFHS) umetoka taarifa ya takwimu za vilabu bora Duniani kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Septemba 22, 2022 hadi Agosti 21 2023.


Upande wa AFRIKA unaonyesha klabu ya YANGA ya Tanzania inashika nafasi ya 3 nyuma ya vilabu vya Ahly ya Misri na Wydad ya Morocco, huku wababe wa Msimbazi Simba SC wakiangukia nafasi ya 12.


Yanga msimu uliopita ilicheza fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na kupoteza kwa klabu ya USM Alger ya Algeria, Mabingwa hao wa CAFCC wanashika nafasi ya 10 kwenye orodha hiyo.


Mabingwa wa African Football League, Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini wako nafasi ya 5 baada ya Pyramid ya Misri huku nafasi ya 6 ikienda kwa FAR Rabat, Raja CA iko nafasi ya 7, Zamalek ya Misri 8 na CR Belouizdad ikiwa ya 9.


Mtandao wa IFFHS umekuwa maarufu sana Tanzania kwa siku za karibuni na kujizolea sifa miongoni mwa mashabiki wa soka kwa namna wanavyoziona klabu zao zikipepea nafasi za juu kwenye takwimu zao.



Nafasi 10 bora Afrika ipo hivi;

1. Al Ahly - Misri

2. Wydad Casablanca - Morocco

3. Pyramids FC - Misri

4. Yanga - Tanzania

5. Mamelodi Sundowns - Afrika Kusini

6. Raja Casablanca - Morocco

7. FAR Rabat - Morocco

8. CR Belouizdad - Algeria

9. Zamalek SC - Misri

10. Esperance - Tunisia.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.