Kimenuka! Panga laondoka na wawili Simba, waambiwa waondoke

 

Kimenuka! Panga laondoka na wawili Simba, waambiwa waondoke


Kimenuka! Panga laondoka na wawili Simba, waambiwa waondoke

Kimenuka! Ndiyo utakavyoweza kusema kwa sasa baada ya Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba kupitisha panga kwa mastaa ili kuingiza maingizo mapya matatu haraka.


Hiyo ikiwa ni siku chache tangu, Simba itoke kufungwa mabao 5-1 na Yanga katika mchezo wa Kariakoo Dabi, uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.


Mara baada ya mchezo huo, shutuma mbalimbali ziliwahusisha baadhi ya wachezaji waidaiwa kucheza chini ya kiwango huku mashabiki wakiwataka mastaa wanaowatuhumu kuachana nao katika usajili wa dirisha dogo litalofungiliwa Januari, mwakani.


Tetesi zinadai kuwa tayari uongozi wa timu hiyo, umempa taarifa kiungo wake mshambuliaji, Mrundi Said Ntibanzokiza ‘Saido’ kutafuta timu nyingine atakayokwenda kuicheze katika dirisha dogo, kutokana na kutokuwepo katika mipango.


Kwa mujibu wa taarifa ambazo tumezipata, katika kikao kilichokaa Jumatatu jioni cha viongozi kwa pamoja wamekubaliana kuwapunguza wachezaji wake nyota walioshuka viwango na wenye umri mkubwa ili kupisha damu changa itakayoleta chanagamoto mpya katika timu.


Mtoa taarifa huyo alisema kuwa hadi kufikia Jumatatu jioni tayari walimalizana na wachezaji wawili wakubwa katika timu, kati ya hao ni Saido huku jina lingine likifichwa kwa ajili ya kufikia makubaliano ya pande mbili.


Aliongeza kuwa panga likipita, uongozi umepanga kukifanyia maboresho kikosi chao katika nafasi tatu kubwa ambazo ni winga, mshambuliaji na kiungo mkabaji.


“Bodi ya Wakurugenzi Simba imepanga kuwapunguza mastaa waliokuwepo katika kikosi chetu cha ili wawapishe wachezaji wengine wapya watakapokuja kuleta changamoto mpya katika timu.


“Na maingizo mapya yapo matatu ya wachezaji wapya wanaokuja kuitengeneza Simba mpya itakayofikia malengo yetu ya msimu huu katika Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Bara.


“Tumepanga kumsajili kiungo mkabaji, mshambuliaji na winga mmoja mwenye uwezo wa kutokea kulia na kushoto, tupo katika mazungumzo ya awali na wachezaji wote hao,” alisema mtoa taarifa huyo.


Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alizungumzia hilo na kusema kuwa:


“Ni lazima uongozi tufanye maamuzi magumu, katika usajili wadirisha dogo, na jukumu hilo tunamuachia kocha wetu mpya atakayekuja kuifundisha timu yetu, kama uongozi tunaamini kabla ya dirisha kufunguliwa kocha atapata nafasi ya kukiangalia kikosi chetu, baada ya hapo tutakaribisha ripoti yake ya usajili.” 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.