Hizi Hapa Jezi Mpya za Timu ya Simba Mechi za Kimataifa
Wekundu wa Msimbazi Simba SC, leo Novemba 22, 2023 wametambulisha jezi mpya ambazo watazitumia kwenye mechi za Kimataifa.
Kwa mujibu wa mitandao yao ya kijamii, uzi huo kutoka Sundaland, unauzwa shilingi 32,000 kwa jumla na shilingi 40,000 kwa rejareja.
Simba wanatarajia kuanza kuuvaa uzi huo Jumapili hii Novemba 25, 2023 watakapoanza mechi yao ya kwanza ya Makundi ya Klabu Bingwa dhidi ya ASEC Mimosas katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.