TETESI: AZIZ K kuwaaga Yanga, Agoma Kuongeza Mkataba

Mkataba wa kiungo mshambuliaji wa Yanga STEPHANIE AZIZI KI mkataba wake unaelekea ukingoni hadi kufikia mwaka kesho mwezi wa sita atakuwa mchezaji huru, Viongozi wa Yanga wamefanya kila linalowezekana ili kumuongezea mkataba mchezaji huyo ila imeshindikana kabisa Kwa kauli yake mwenyewe AMEGOMA kwa herufi kubwa akisema hataki kusalia ndani ya timu hiyo.

MZEE WA ZA CUBA DOCTOR MOHAMEDI HAMISI nimefanya jitihada za kuutafuta uongozi wa mchezaji huyo na kufanya nao mazungumzo na kisha kukiri kuwa hawana mpango tena wa kusalia ndani ya Klabu hiyo yenye maskani mitaa ya Twiga na Jangwani huku nikiwauliza kama wapo tayari kusalia Tanzania 🇹🇿 lakini kwenye timu tofauti wakajibu ndio inawezekana kama timu hiyo itakuja na offer nzuri mezani inayoridhisha wao kama wasimamizi wa mchezaji wanaangalia maslahi ya mchezaji wao kwanza kisha mengine yanafuata.

Uongozi wa Yanga kwa sasa unahaha kutafuta kiungo mshambuliaji mwingine ambaye atakuja kurithi nafasi ya AZIZI KI mara baada ya kuondoka klabuni hapo kwakuwa juhudi za kumzuia asiondoke Klabuni hapo zikiwa zimegonga mwamba kila la kheri AZIZI KI 👋👋

Je unahisi AZIZI KI anataka kwenda timu gani?🤪
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad