Simba Wameumaliza Mwendo African Football League, Al Ahly Wawakazia

 

Simba Wameumaliza Mwendo African Football League, Al Ahly Wawakazia

Wawakilishi wa Tanzania katika Michuano ya African Football League, Timu ya Simba SC imetupwa nje ya michuano hiyo baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Al Ahly nchini Misri.


Mchezo huo wa robo Fainali mkondo wa pili umepigwa katika Uwanja wa Kimataifa wa Cairo na kuishuhudia Ahly ikivuka hatua ya Nusu Fainali kwa faida ya magoli mengi ya ugenini baada ya kutoka sare ya magoli 2-2 mchezo wa mkondo wa kwanza.


Matokeo ya jumla ya mchezo huo ni sare ya magoli 3-3 lakini Ahly wanasonga kwa faida ya kufunga magoli mengi ugenini.


Katika mchezo uliopigwa leo Simba walijikuta muda mwingi wa mchezo wakizuia baada ya Al Ahly kuonekana kuingia katika mchezo huo wakisaka ushindi tangu dakika ya kwanza ya mchezo.


Goli la Simba leo limefungwa na Sadio Kanoute dakika ya 67 ya mchezo kabla ya Ahly kusawazisha dakika ya 75 kupitia kwa Mahamoud Kahraba.


Je una neno gani la kuwaambia Simba SC? Tupe maoni yako

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.