Kuelekea AFCON 2027, Waziri wa Kenya Atoa Maagizo Kwa Tanzania

 

Kuelekea AFCON 2027, Waziri wa Kenya Atoa Maagizo Kwa Tanzania

Waziri wa Michezo nchini Kenya, Ababu Namwamba amezitaka timu za taifa za nchi za Afrika Mashariki kujiandaa vizuri kwa ajili ya Fainali za Mashindano ya 36 ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) zitakazofanyika katika nchi hizo.

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) lilizitangaza Tanzania, Kenya na Uganda kushinda zabuni ya kutaka kuandaa kwa pamoja fainali hizo.

Waziri huyo amesema hayo baada ya kuwasili kutoka Cairo, Misri ambako walishinda ombi lao la Ê»Pamoja Bid’.

“Kama waandaaji wa mashindano haya, tunatarajia kufanya mambo mengine ikiwemo kujenga vikosi imara ndani ya ukanda wetu. Hatutaki kuongeza wingi. Tunataka kutoa ushindani na kweli na kufika mbali,” amesema Ababu.

“Hiyo ikiwa na maana kuwa Harambee Stars, Taifa Stars na ile ya Uganda, the Cranes lazima waanze maandalizi ya nguvu kama vile hawajawahi kufanya hivyo kwa ajili ya kutoa ushindani wa aina yake,” ameongeza.

Ababu ameelezea jinsi mashindano hayo yatakavyoendeleza vipaji katika nchi za Afrika Mashariki.

“Kuandaa mashindano haya ni njia moja ya kuendeleza vipaji vya soka, kuendeleza miundombinu ya soka, na kuanzisha utamaduni wa kuwa sehemu ya utamaduni huu wa kuandaa mashindano makubwa,” amesema Ababu.

Ameongeza kusema kuwa nchi hizo tatu zitanufaika na ujenzi na ukarabati wa miundombinu.

Rais wa CAF, Patrice Motsepe juma lililopita aliitangaza Afrika Mashariki kushinda ‘Pamoja Bid’ kwa ajili ya kuandaa kwa pamoja fainali hizo za AFCON 2027.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad