Eng. Hersi Aichambua Yanga ya Sasa na Yanga iliyopita

Eng. Hersi Aichambua Yanga ya Sasa na Yanga iliyopita


Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema kuwa timu yao imekwenda kwenye hatua ya Makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, si kwa bahati mbaya bali ni kutokana na mipango waliyoiweka.


Hersi amesema kuwa Yanga inakwenda kupambana kwenye michuano hiyo ili kufikia hatua kubwa na kuweka alama na heshima na si kushiriki tu kama ambavyo vilabu vingi vimekuwa vikifanya.


“Yanga sisi tumekuwa na mafanikio ya hatua. Mwaka 2020 wakati tulikuwa tunaingia na wadhamini wetu wakiwa GSM wakipambana kuirudisha hadhi ya yetu, ilikuwa ni kuanza kuijenga timu. Yanga katika kila idara kulikuwa na mapungufu au madhaifu.


“Ukizungumzia benchi la ufundi lilikuwa na mapungufu sana, ubora wa wachezaji ulikuwa wa wastani sana, upande wa uongozi pia hata kwa wadhamini tulikuwa na mdhamini mmoja tu SportPesa, hayo yote yalikuwa yanatufanye tudumae hata kwenye mafanikio.


“Baada ya kuingia tukasema lazima tuirudishe Yanga kwenye mafanikio, tukaanza kuboresha idara moja baada ya nyingine. Leo miaka mine mafanikio ni makubwa, kuanzia benchi la ufundi kocha mkuu, msaidizi, fitness coach, physio, kocha wa makipa, daktari hilo tumeboresha.


“Upande wa wachezaji, tazama kikosi cha Yanga cha sasa na miaka michache iliyopita, utaone akuna maboresho kwenye kila eneo. Mchezaji wa Yanga ambaye hapati nafasi ya kuanza kila mechi akienda timu nyingine anaanza na anaweza kupewa kitambaa cha unahodha.


“Ukija kwenye uongozi, CEO, wakurugenzi wa idara kadha wa kadha, utaalam kwenye idara ya habari kuna ubora mkubwa na tumeongeza vijana wanaofanya kazi kwa kujituma na tukawaongezea vifaa. Mwezi uliopita yanga imepata intereactions ya zaidi ya watu milioni 10 na kuwa namba moja Afrika, hawa watu hawaji kwa sababu tu social media zipo, wanakuja kwa sababu kuna contents bora.


“Upande wa masoko tumeleta wadhamini wengi sana na wanaridhika kwa namna ambayo Yanga inawapa thamani yao. Na sasa hivi nakwambia exclusively kwamba tunakwenda kusaini mikataba na makampuni mawili ndani ya wiki mbili zijazo.


“Kwa hiyo mafanikio ya Yanga yanajengwa na kila idara ndiyo maana unaona leo tunakwenda kufanikiwa kutinga hatua ya makundi,” amesema Eng. Hersi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.