Robertinho Kifua Mbele, Awapa Tano Mastaa Wake, Uongozi Kicheko

Robertinho Kifua Mbele, Awapa Tano Mastaa Wake, Uongozi Kicheko

 Robertinho Kifua Mbele, Awapa Tano Mastaa Wake, Uongozi Kicheko

Kocha mkuu wa Simba, Roberto Oliveira 'Robertinho' amesema amefurahishwa na kiwango cha nyota wake kilichoendana na matokeo ya ushindi dhidi ya Tanzania Prisons.


Simba ambayo licha ya kufuzu ligi ya mabingwa Afrika, baadhi ya mashabiki walionesha kutoridhishwa na kiwango cha timu kufuatia matokeo ya sare katika mechi mbili za ligi hiyo dhidi ya Power Dynamos.


Leo Wekundu hao wakicheza kwa ubora wao, walionekana kutulia licha ya kutanguliwa kufungwa bao dakika ya 12 kupitia kwa Edwine Balua kabla ya kusawazisha dakika ya 34 kupitia kwa Clatous Chama na John Bocco dakika ya 45 huku Saido Ntibazonkiza akihitimisha karamu ya mabao kwa penalti.


Akizungumza baada ya mchezo huo, kocha huyo raia wa Brazil amesema amekoshwa na kiwango cha vijana wake na matokeo mazuri waliyopata.


"Ni matokeo mazuri tunapanda kileleni, haikuwa mechi rahisi lakini vijana wameonesha soka safi na kiwango bora, tunaenda kujipanga na mchezo ujao" amesema Robertinho.


Kwa upande wake Meneja Habari na mawasiliano wa timu hiyo, Ahmed Ally amesema hii ni rekodi ya kwanza kwao kupata ushindi mnono wa idadi hiyo ya mabao kwani mara kadhaa ushindi wao kwa Prisons huishia mawili, moja au sare.


Amesema wamefurahishwa na matokeo hayo na kwamba wanaenda kupambana kuhakikisha wanabaki kileleni japokuwa haitakuwa kazi rahisi kwani ligi bado haijafika popote.


"Ni mechi nne tu hivyo hatuwezi kutamba kutoshuka kileleni, kimsingi ni kuendelea kuweka mipango na kupambana kwa wachezaji ili kulinda nafasi hii, Prisons hutupa sana upinzani lakini tunashukuru kwa matokeo haya" amesema Ally.


Jambo ambalo lilionekana kuwavutia Simba chini ya kocha Robertinho ni kuwapo kwa shabiki ambaye ni mtu mwenye ulemavu Aiwelo Simon na kuamua kupiga naye stori, huku kocha wa makipa wa timu hiyo, Daniel Cadena akimpa zawadi ya fedha ambayo haikujulikana haraka kiasi chake

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.