Robertinho Atamba Kuifunga Al Ahly Bao za Kutosha, Aweka Mtego Huu Kwa Mkapa

 

Robertinho Atamba Kuifunga Al Ahly Bao za Kutosha, Aweka Mtego Huu Kwa Mkapa

KOCHA Mkuu wa Simba, Mbrazili, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema hana hofu ya kukutana na Al Ahly ya Misri, kwani anazijua mbinu zote wanazotumia.

Timu hizo zinatarajiwa kukutana katika mchezo wa kwanza wa CAF African Football League unaotarajiwa kucheza Oktoba 20, mwaka huu.

Mchezo huo wa robo fainali ya kwanza unatarajiwa kupigwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kabla ya kwenda kurudiana Misri.

Akizungumza na Spoti Xtra, Robertino alisema kuwa mara baada ya droo ya michuano hiyo kuchezeshwa na wao kukutana na Al Ahly, haraka alianza kuwafuatilia kwa karibu wapinzani wao hao.

Robertino alisema amewafuatilia kwa kupitia video za michezo ambayo wameicheza msimu huu kwa lengo la kuwafahamu wachezaji hatari, hivyo tayari amewafahamu.

“Wapinzani wetu Al Ahly wana wachezaji wengine wazuri na hatari wa kuchungwa, lakini hiyo hainifanyi niwaogope, kwani na sisi tuna wachezaji wakubwa na hatari,” alisema Robertinho.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.