Yanga vs Al Merreikh |
Kete Tatu Zaibeba Yanga Kwa Al Merreikh ya Sudan
Wawakilishi wa Tanzania katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Young Africans wakiwa kwenye maandalizi ya kuwakabili Waarabu wa Sudan, zimetajwa sababu tatu zitakazowapa ushindi mbele ya Al Merreikh.
Ni Kocha Mkuu wa Al Merreikh ya Sudan Osama Nabieh ameweka wazi sababu hizo kwa kubainisha kuwa ana mtihani mzito mbele ya Young Africans kutokana na ubora wa kikosi cha Wananchi.
Al Merreikh wanatarajiwa kukutana na Young Africans katika mchezo wa kufuzu makundi ya Ligi ya Mabingwa Septemba 16 katika Uwanja wa Pele nchini Rwanda.
Akizungumza kuelekea mchezo wao unaofuata dhidi ya Young Africans kocha huyo aliitaja sababu ya kwanza kuwa: “Tunatarajia kukutana na upinzani mgumu kutoka kwa Young Africans kuwa kwenye ubora wao mkubwa ambao wamekuwa wakiuonyesha katika michuano ya kimataifa katika siku za karibuni.
“Pili wenzetu wanapata faida kubwa ya kucheza michezo ya ligi kuu ambapo inawapa uwezo mkubwa wa kujijenga zaidi na kufahamu wapi kuna mapungufu na wapi kunatakiwa kufanyiwa maboresho.
Sababu ya tatu kocha huyo alibainisha kuwa: “Malengo yetu ni kuona tunafika makundi kama msimu uliopita, sisi tunayo changamoto ya kukosa mechi nyingi lakini naamini tunayo nafasi nzuri ya kufanya vyema dhidi yao na kutimiza malengo yetu,” amesema Nabieh.