Ahmedy Ally Atamba : Sio Al Ahly tu Mleteni Yoyote Tunamfunga nje Ndani

 

Ahmedy Ally Atamba : Sio Al Ahly tu Mleteni Yoyote Tunamfunga nje Ndani

Uongozi wa Simba umesema kuwa licha ya kupangiwa kukutana na Al Ahly bado kwao hawakuwa wanahofia kukutana na timu yoyote kwani walikuwa tayari kukytana na timu yoyote kutokana na ukubwa wao.

Akizungumzia hilo Afisa Habari wa Simba Ahmedy Ally alisema kuwa “Sisi wakati drooo inapangwa tulifahamu kuwa tunakwenda kukutaa na timu kubwa kwa maana ya wakubwa wenzetu hivyo tayari tulikuwa tunalifahamu hilo.

Kwahiyo ndio maana baada ya kupangiwa Al Ahly uliona tulishangilia kwasababu hata kama tungepangiwa Waydad Casablanca au Mamelod Sundwons bado tungeweza kushangilia zaidi.

“Jambo ambalo lipo kwa sasa mbele yetu ni kuhakikisha kuwa tunafanikiwa kusonga mbele kuiandaa kwaajili ya kupambana na Al Ahly na tuseme tu kuwa wanafahamu mziki wetu uwa ni mkubwa na tutawashangaza,” alisema kiongozi huyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.