Nyota wa Al Nassr ya Saudi Arabia, Cristiano Ronaldo, Sadio Mane na wachezaji wengine wa klabu hiyo kama Talisca wameonekana kwenye video wakiwa wamevalia mavazi ya kitamaduni ya taifa hilo. Ronaldo (38) alijiunga na timu hiyo tangu mwaka jana lakini tayari ameshayazoea maisha ya Saudia na tamaduni zake. Ronaldo na Mane wamekuwa gumzo kubwa mitandano baada ya kuibuka wakiwa wamevalia mavazi yenye tamaduni ya taifa hilo huku pia wakiwa wameshika mapanga. Ronaldo alivaa kanzu nyeupe na joho jeusi wakati Mane alivaa joho la rangi ya dhahabu na kanzu nyeupe na hiyo yote ni ilikuwa katika kuadhimisha sikukuu ya kitaifa ya Saudi ambapo Video hiyo itapamba sherehe hizo zitakazoisha wiki ijayo.
Cristiano Ronaldo, Sadio Mane Wazua Jambo Saudi Arabia
0
September 25, 2023