Fiston Mayele "Nimempa Kocha Anachokitaka"

 

Fiston Mayele "Nimempa Kocha Anachokitaka"

 Fiston Mayele "Nimempa Kocha Anachokitaka"

Straika wa zamani wa Yanga anayekipiga Pyramids ya Misri, Fiston Mayele ameanza kutupia mabao matatu kwenye mechi za kirafiki ilipoifumua Varska Antalya ya Uturuki mabao 7-0, huku akisema hat trick hiyo imemuongezea kujiamini kikosini.


“Sio mechi ya mashindano, lakini kufunga tu kwangu ni mwanzo mzuri. Nimejiongezea kujiamini pia nimempa kocha alichokuwa anakitarajia kutoka kwangu,” alisema Mayele.


“Nimepokewa vizuri napewa ushirikiano mzuri na kufunga kwangu kumeongeza kitu kwenye uwepo wangu ndani ya timu hili. Kwangu ni jambo zuri na naamini nina nguvu ya kuamini kuwa kila kitu kinawezekana.”


Mayele alisema mechi za maandalizi ya msimu ndizo zinatoa mwanga kwa kocha kupata kikosi ambacho kitamsaidia, hivyo anapambana kuhakikisha anaingia kikosi cha kwanza.


“Naamini uwezo wangu naweza kuingia kikosini lakini ni suala la muda na kuendelea kumshawishi kocha ili aweze kuniamini nimpe kitu nilichonacho," amesemaMayele.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.