Mbwana Samatta Bado Sana Yupo Kwenye Mpira Hajamaliza

 

Mbwana Samatta Bado Sana Yupo Kwenye Mpira Hajamaliza

Wakati wadau na mashabiki wa soka la Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki wakimwona nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta 'Samagol' anamaliza kutokana na umri kumtupa mkono kwake ni tofauti anaona bado ananafasi ya kuendelea kupiga hatua.


Mshambuliaji huyo ambaye anashikilia rekodi kibao kwenye uchezaji wake wa soka la kulipwa barani Ulaya, alisema kwenye mahojiano maalumu ambayo alifanya na Millardayo, anajiona kuwa bado anaweza kuendelea kucheza soka la ushindani barani humo tofauti na anavyochukuliwa.


Licha ya msimu uliopita kuichezea KRC Genk kwa mkopo akitokea Fenerbahce ya Uturuki, Samatta mwenye miaka 30, alisema; "Maisha yangu yamekuwa kama ndege najaribu kwa kadri ya uwezo wangu kucheza ili nikimaliza muda wangu niseme kweli nilipambana na naendelea kujipigania."


Samatta anasema kwasababu mkataba wake na Fenerbahce umebaki mwaka mmoja atalazimika kurudi klabuni hapo ili kumaliza mkataba wake.


Hata hivyo anasema viongozi wa klabu hiyo watachagua kati ya kumuuza katika kwingine au kumbakiza amalizie mwaka uliosalia.


"Kuhusu kuondoka Genk bado mimi ni mchezaji wa Fenerbahce mkataba wangu unamalizika 2024 kwahiyo naweza kusema nitarudi Fenerbahce na wao kama klabu watachagua kama kuniuza wapate pesa au wanibakize ili kumalizia mkataba wangu."


ISHU YA UBINGWA


Anasema baada ya kukosa ubingwa ambao walitarajia kuuchukua kwa ambao ulisalia point moja pekee Kocha Wouter Vrancken alikaa na wachezaji na kuwaambia yamepita na waangalie msimu ujao.


Kocha huyo alioona kukaa na mastaa hao na kupunguza presha yao na kuwaeleza kuwa walifanya walichotakiwa kufanya na bahati haikuwa upande wao.


"Ligi ya Ubelgiji iko tofauti kidogo na nyingine kwasababu kuna baadhi ya sheria ndio zilitubana ikiwemo kukatwa point na kama Genk tulistahili kubeba ubingwa lakini kutokana na bahati yetu kuwa mbaya tukaikosa." alisema Samatta


OFA TATU MEZANI


Anasema kuelekea msimu ujao tayari kuna vilabi mbalimbali barani humo na mabara mengine yanahitaji huduma yake lakini kitokana na muda kutokuwa sahihi hatoweka wazi timu hizo.


Ukiachana na Ulaya ambapo anacheza kwasasa lakini mabara mbalimbali ikiwemo bara la Amerika na Uarabuni.


"Tayari nina ofa kutoka vilabu mbalimbali lakini sipendi kuvitaja kwasababu sio muda sahihi ila kiufupi ninazo kutoka bara la ulaya, America na uarabuni,"


ANATAMBULIKA HUKO


Mbali na kucheza kwa mafanikio lakini anakutana na maswali mengi kuhusu nyota wengine wa Kitanzania ambao wamewahi kucheza soka barani humo.


"Wakati naenda zangu Genk waandishi nchini humo waliwahi kuniuliza kama kuna mchezaji wa kitanzania ambae aliwahi kucheza Ulaya nikawaambia kuwa yupo ambae ni Mzee Sunday Manara lakini kwa kipindi hicho wachezaji wengi walikuwa hawajazaliwa na wengine ni wadogo,"

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.