Mbwana Samatta Apewa THANK You na KRC Genk, Kujiunga na Timu Hii ya Ugiriki
Nahodha wa timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) Mbwana Samatta amejiunga na klabu ya PAOK ya Ugiriki akitokea klabu ya Fenerbahce aliyovunja nayo mkataba.
Samatta aliyekipiga KRC Genk msimu uliopita akiwa kwa mkopo akitokea Fernabache amejiunga na PAOK ambao msimu ujao watashiriki mashindano ya Europa.
PAOK wameweka taarifa ya Samatta kujiunga na timu yao, lakini hawajaandika amejiunga na mkataba wa muda gani.