Matokeo ya Mchezo wa Kirafiki Turan PFK vs Simba


Matokeo ya Mchezo wa Kirafiki Turan PFK vs Simba

Matokeo ya Mchezo wa Kirafiki Turan PFK vs Simba  

Klabu ya Simba imepoteza mechi ya Kwanza katika kambi yake ya kujiandaa na msimu mjini Ankara nchini Uturuki baada ya kuchapwa 1-0 na Turan FK ya Turkmenistan, bao la dakika ya nne la Roderik Miller jioni ya leo.

Huo ulikuwa mchezo wa marudiano baina ya timu hizo baada ya mchana wa leo Simba kushinda 2-0, mabao ya Kibu Dennis na Nahodha, John Raphael Bocco.

Kwa ujumla Simba imekwishacheza mechi nne kwenye kambi yake ya kujiandaa na msimu nchini Uturuki baada ya sare ya 1-1 na Zira FK ya Azerbaijan Julai 24.

Turkmenistan ni nchi inayopatikana Asia ya Kati ikiwa imepakana na Kazakhstan upande wa Kaskazini Magharibi na Uzbekistan kwa Kaskazini Mashariki, ambayo kwa sasa inashika nafasi ya 138 kwenye renki za FIFA ikiwa chini ya Tanzania ambayo ipo nafasi ya 123

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.