Ukweli Kuhusu Simba Kumtema Mchezaji OKRAH, Mademu na Pombe Vyahusishwa

 

Ukweli Kuhusu Simba Kumtema Mchezaji OKRAH, Mademu na Pombe Vyahusishwa

Uongozi wa klabu ya Simba umetangaza rasmi kuachana na kiungo wake mshambuliaji Augustine Okrah baada ya kumalizika Msimu wa mashindano wa 2022/23.

Okrah raia wa Ghana amemaliza mkataba wake ndani ya klabu hiyo na mchezaji huyo hatoongezewa mkataba mpya.

Okrah alijiunga na Simba mwanzoni kwa msimu huu akitokea Benchem United ya nyumbani kwao Ghana ambapo ameonyesha uwezo mkubwa katika mechi zote alizocheza.

Katika msimu mmoja aliohudumu ndani ya kikosi cha Simba Okrah amekuwa na mchango mkubwa akicheza mechi 17 na kufunga mabao manne na kusaidia kupatikana kwa jingine moja.

Aidha Staa huyo atakumbukwa kwa kufunga goli kwenye mechi dhidi Yanga ambapo alishangilia mpaka kuvua jezi yake, ukichilia mbali kukosa nafasi nyingine muhimu ambazo zingeweza kuipa Simba ushindi wakati huo.

Hata hivyo, taarifa za ndani zaidi zinadai kuwa Simba wameshinwa kuendelea na nyota huyo, kutokana na tabia zake za nnje ya uwanja, ambapo inadaiwa amekuwa mlevi na mtu wa kupenda starehe za wanawake kupitiliza, huku suala la yeye kuwa majeruhi likichangia kwa kiasi kikubwa.

Kuondoka kwa Okrah ni ishara ya kuanza rasmi utelekezaji wa maboresho ya kikosi cha Simba kuelekea msimu ujao wa mashindano.

Uongozi wa klabu hiyo umedhamiria kufanya maboresho makubwa kwenye kikosi kuanzia eneo la benchi la ufundi kwa kuongeza watalaamu zaidi pamoja na wachezaji wenye hadhi kubwa na ubora wa kuitumikia Simba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad