Rais Samia Aendelea Kumimina Neema Yanga...Ahadi Nyingine Mpya Hii Hapa

 

Rais Samia Aendelea Kumimina Neema Yanga...Ahadi Nyingine Mpya Hii Hapa

Rais Samia Suluhu Hassan ameilipia klabu ya Yanga ndege maalumu ya kuwapeleka mkoani Mbeya kucheza michezo yao miwili ya Ligi Kuu Bara kutokana na mwingiliano wa ratiba.

Jana Juni 4, 2023 Rais Samia aliwaalika Yanga chakula cha jioni Ikulu leo Jumatatu ambapo ratiba hiyo iliingiliana na safari ya klabu hiyo kuelekea mkoani Mbeya.

Akizungumza katika radio ya Wasafi jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Juni 5, 2023 Rais wa klabu hiyo, Hersi Said amesema kutokana na mwingiliano huo wa ratiba uliotokea Rais Samia ameilipia Yanga ndege maalumu kuwapeleka Mbeya baada ya chakula cha jioni.

“Ndege yetu ambayo tulitakiwa kuondoka nayo kwenda Mbeya ilikuwa ni saa 1 usiku lakini kwasababu ya mwaliko wa Rais Ikulu leo jioni tulimpa taarifa kuhusu safari yetu na sasa amelipia ndege maalumu kutupeleka Mbeya,”amesema Hersi.

Hersi amesema ndege hiyo iliyolipiwa na Rais Samia itaondoka saa 5 usiku baada ya kumaliza mazungumzo na chakula cha jioni

“Akasema nyinyi vijana wangu njooni kwa ajili ya chakula cha jioni tutazungumza na baada ya hapo sasa ndege maalumu itawapeleka Mbeya,” amesema

Yanga ambaye ni bingwa mara 29 wa Ligi Kuu Bara atakuwa mkoani Mbeya katika mechi dhidi ya Mbeya City itakayopigwa kesho Juni 6, na kumalizia na Tanzania Prisons Juni 9, 2023.

Yanga imepata mwaliko huo na Rais Samia baada ya kumaliza mshindi wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) mwaka 2022/2023.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.