Feisal Salum 'Kabla ya Mgogoro Nilimpigia Sana Simu Boss Ghalibu GSM Tuyamalize Akawa Hapokei Simu Yangu'

Feisal Salum 'Kabla ya Mgogoro Nilimpigia Sana Simu Boss Ghalibu GSM Tuyamalize Akawa Hapokei Simu Yangu'


“Nilimpigia simu Ghalibu [GSM] akawa hapokei, nikituma sms hajibu, nikawa nahisi pengine ana kazi zake akipata muda atanitafuta. Badae nikajua simu zangu anaziona na sms anasoma lakini hazishiki.”


“Wakati huo nilikuwa namtafuta kabla ya huu mgogoro kuanza ili nimshirikishe kutafuta suluhu lakini alikuwa hanipi ushirikiano. Na sikuwahi kumpata.”


“Hili sakata lilipotokea akaanza kunipigia simu, hata ungekuwa wewe ungepokea simu yake? Wakati wewe unampigia ili kupata suluhisho yeye hapokei simu zako, sakata limekuwa bichi yeye ndo anapiga simu. Roho inaniuma hadi kesho!


“Mimi masikini sina kitu, hata kama una hela zako usinidharau. Kipaji changu ndio kinaniweka mjini. Hata kama unanidharau, kipaji alichonipa Mungu ndio kinakufanya wewe utangaze mambo yako.”


- Feisal Salum via #PowerBreakFast @cloudsfmtz

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad