Shiza Kichuya Aweka Wazi Dhamira yake ya Kurudi Simba SC

 

Shiza Kichuya Aweka Wazi Dhamira yake ya Kurudi Simba SC
Shiza Kichuya

Kiungo aliyewahi kutamba katika klabu za Mtibwa na Simba kwa sasa akiwa anakipiga kwenye klabu ya Namungo Shiza Kichuya ameweka wazi matamanio yake ya kurejea timu kubwa ikiwemo Simba aliyowahi kutamba nayo. Kichuya Afunguka Kurudi Tena Simba


Kichuya ambaye amefanya vizuri na kuwa mchezaji tegemeo na muhimu wa Namungo wa misimu miwili na kufanya vizuri na kuwahi kuibuka tetesi kuwa huenda akarejea tena mitaa ya Kariakoo na Msimbazi na kujiunga na Yanga au Simba.


Kichuya aliweka bayana kila kitu na kusema kuwa haikuwa rahisi kufika alipo sasa au kurudi kwenye ubora kiasi cha kuhusishwa kurejea Simba au kwenda timu kubwa na kusema kuwa bado yupo Namungo. Kichuya Afunguka Kurudi Tena Simba


“Mimi nashukuru kuwa watu wameona kila ambacho nimefanya kwa misimu miwili nikiwa Namungo na kuibuka kwa stori hizo za kurudi Simba na kwenda timu nyingine kubwa zaidi.”


Niseme ukweli, haikuwa rahisi, nilipitia kipindi fulani kigumu kabla ya kuinuka tena, hakuna mchezaji asiyependa kucheza timu kubwa, lakini mimi kwa sasa bado nipo Namungo na nina mkataba wa mwaka mmoja hapo. Alisema Kichuya

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.