Okwa Atapika Nyongo 'Kocha hapangi kikosi Simba kuna mtu anakuja na orodha'

  

Okwa Atapika Nyongo 'Kocha hapangi kikosi Simba kuna mtu anakuja na orodha'
Nelson Okwa

Aliyekuwa kiungo wa Simba SC, Nelson Okwa amefunguka juu yaliyokuwa yakijiri klabuni hapo ambapo amefichua kuwa wachezaji hawachezeshwi kulingana na utendaji wao mazoezini bali ‘yupo mtu ambaye huja na orodha ya wachezaji wanaotakiwa kucheza na wasiotakiwa kucheza bila kujali ni nini wamekifanya kwenye uwanja wa mazoezi.’


Akizungumza na kituo cha habari cha G&T Online TV, Okwa amesema, "Wakati Kocha Zoran akiwa Simba ilikuwa mchezaji unacheza kulingana na ulivyo-perfom kwenye mazoezi.


"Lakini baada ya kuondoka ikawa kama Kuna watu wanaleta Orodha ya wachezaji wanaotakiwa kucheza na hawa wasicheze bila kujali ni nini wamekifanya kwenye uwanja wa mazoezi," amesema Okwa.


Ikumbukwe kuwa Okwa ambaye ni raia wa Nigeria alikuwa mchezaji wa Simba ambaye akisajiliwa ndani ya kikosi hicho mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Rivers United ya nchini kwao lakini baadaye kiwango chake kilionekana hakiwaridhishi mabosi wa SImba ambapo walimpeleka kwa mkopo Ihefu FC.


Baada ya msimu kumalizika, Okwa alipewa mkono wa kwa heria akiwa amecheza mechi chache jambo ambalo amesema hakupewa muda kuonyesha kiwango chake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.