Onyango Aomba Kuondoka Simba Aandika Barua Kwa Uongozi

 

Onyango Aomba Kuondoka Simba Aandika Barua Kwa Uongozi

BEKI wa kati mkongwe wa Simba raia wa Simba, Joash Onyango, ameona isiwe shida, haraka ameandika barua kwa uongozi akiomba kuondoka mwishoni mwa msimu huu.


Mkenya huyo ni kati ya wachezaji ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa huu, huku Simba ikiwa imeanza mazungumzo na baadhi ya warithi wake.


Kati ya warithi wake, yupo anayetajwa sana ambaye ni Abdul Rwatubyaye anayeichezea Timu ya Taifa ya Rwanda na Klabu ya Rayon Sports ya nchini Rwanda.


Taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, Onyango, juzi Jumanne aliandika barua hiyo kwa uongozi akiomba aondoke na kutokuwepo sehemu ya wachezaji watakaoichezea timu hiyo msimu ujao.


Mtoa taarifa huyo alisema, sababu kubwa ya Onyango kuomba kuondoka hapo, ni kuchoka kuandamwa na mashabiki wa timu hiyo, kila timu inapopata matokeo mabaya.


“Onyango ameandika barua ya kuomba kutoongezewa mkataba wa kuendelea kuichezea Simba mara baada ya mkataba wake kumalizika.


“Kikubwa kilichomfanya aandike barua hiyo ya kuomba aondoke mwenyewe ni kuchoshwa na kuandamwa na maneno kutoka kwa mashabiki kila timu inapopata matokeo mabaya.


“Tangu muda mrefu amekuwa akichukizwa na hicho kitendo, lakini mara baada ya mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Azam FC ambao walitufunga mabao 2-1, alichukizwa zaidi baada ya mashabiki kumuandama peke yake,” alisema mtoa taarifa huyo.


Alipotafutwa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, kuzungumzia hilo, alisema: “Sina taarifa hiyo rasmi kutoka kwa uongozi, tusubirie muda ukifika tutaweka wazi.”


STORI NA WILBERT MOLANDI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.