Newcastle Wadhamiria kumng’oa Mchezaji Neymar PSG

 

Neymar PSG
Neymar PSG

Imeelezwa kuwa Sehemu kubwa ya wenye hisa katika klabu ya Newcastle United wameonesha nia ya kumsajili Mshambuliaji kutoka Brazil na Paris Saint-Germain (PSG), Neymar da Silva Santos Júnior.

Kundi la wamiliki wenye hisa nyingi (PIF) wanataka Newcastle kufanya usajili mkubwa katika kipindi hiki cha majira ya joto na wanaamini wanaenda kumaliza msimu katika nne bora na kufuzu kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na kutumia faida hiyo.

Uhamisho unaowezekana kwa Cristiano Ronaldo pia umejadiliwa na PIF na wana mawasiliano ya moja kwa moja na klabu yake ya sasa ya Al-Nassr, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 hafikiriwi na kocha wa Newcastle, Eddie Howe.

Vyanzo vya habari vimedai kuwa licha ya nia ya kumtaka Ronaldo, kamwe hawatamlazimisha mchezaji yeyote katika kikosi cha kocha, ambacho yeye na benchi lake la ufundi hawana mpango naye. Hata hivyo, Neymar ni suala tofauti.


Newcastle iko sokoni ikimsaka mshambuliaji wa kushoto kabla ya msimu ujao ili kuimarisha kikosi chao wakati wakijiandaa kurejea katika Ligi ya Mabingwa.

Neymar mwenye umri wa miaka 31 anaonekana anafiti kabisa katika kikosi hicho, huku tayari kukiwa na muunganiko mzuri wa Wabrazil pamoja na Bruno Guimaraes na Joelinton wachezaji wawili maarufu sana katika timu hiyo msimu huu.

PSG iko mbioni kumpiga bei Neymar katika kipindi cha majira ya joto, huku wengi wakifikiria kuwa kama ni uvunjifu wa tamaduni katika klabu hiyo, huku Lionel Messi akithibitishwa kuondoka baada ya kwenda Saudi Arabia bila ruhusa.

Neymar amekuwa na PSG tangu mwaka 2017 wakati walipoilipa Barcelona kiasi cha Euro milioni 222, ambacho kilikuwa rekodi ya usajili kwa wakati huo.

Manchester United, Manchester City na Chelse nao pia wamehusishwa na kutaka kumsajili mchezaji huyo, huku ikiaminika kuwa klabu hizo kubwa katika Ligi Kuu zimekuwa zikimfuatilia mchezaji huyo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.