Mshambuliaji wa PSG, Lionel Messi Kutimkia Saudi Arabia, Mkataba Mnono

Mshambuliaji wa PSG, Lionel Messi Kutimkia Saudi Arabia, Mkataba Mnono


Mshambuliaji wa PSG, Lionel Messi Kutimkia Saudi Arabia, Mkataba Mnono


Mshambuliaji wa PSG, Lionel Messi ameripotiwa kuwa tayari amefikia makubaliano kuhamia Saudi Arabia, Hata hivyo klabu ambayo Muargentina huyo atachezea haijawelwa wazi lakini inaelezwa kuwa utakuwa mkataba mnono kwa mujibu wa AFP.

"Messi ameshamalizana. Atacheza Saudi Arabia msimu ujao, Mkataba ni wa kipekee. Ni mkubwa. Tunakamilisha mambo madogo," kiliongeza chanzo hicho

Messi (35) anahusishwa na Klabu ya Al Hilal, baada ya kusimamishwa na PSG wiki iliyopita kwa kufanya safari ya kwenda Saudi Arabia bila idhini ya klabu hiyo ya ligi kuu u

Klabu ya PSG ilipoulizwa kuhusu ripoti hizo imesema kwa sasa Messi ni mchezaji wa Paris Saint-Germain na kubainisha kwamba anasalia chini ya mkataba hadi Juni 30.

Ikiwa uhamisho huo utafanikiwa basi mshindi huyo mara 7 wa Ballon D'or atafuata nyayo za mpinzani wake wa muda mrefu Cristiano Ronaldo, ambaye alijiunga na klabu ya Saudi Pro League ya Al Nassr kwa mkataba mkubwa mwezi Januari.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.