CAF Super League yaishurutisha Simba SC kusajili

Published from Blogger Prime Android App

Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Imani Kajula amesema wamejipanga kufanya usajili mkubwa baada ya kushindwa kufanya vizuri msimu huu kwa lengo la kuboresha kikosi hicho kinachotarajia kushiriki michuano ya CAF Super League.

Simba SC ni klabu pekee kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki, itakayoshiriki michuano hiyo mikubwa Afrika ambayo inatarajiwa kuanza mwezi Oktoba mwaka huu.

Kajula amesema: “Akili na nguvu zetu ni kuboresha kikosi kwa ajili ya Super League, Simba ni miongoni timu nane katika Bara la Afrika itakayoshiriki michuano hiyo, lazima tufanye usajili mzuri kwa kuboresha kikosi chetu, sasa tunafanya kazi kwa vitendo na si maneno.

“Tumeona msimu huu hatukufanya vizuri, tumeona tatizo la kufanyiwa kazi haraka, tunakutana na mkuu wa benchi la ufundi kwa ajili ya tathmini ya kikosi na mwenendo wa msimu huu na kujadili msimu ujao,”


Klabu nyingine zitakazoshiriki Michuano ya CAF Super League ni Mamelodi Sundowns, (Afrika Kusini), Petro de Luanda (Angola), TP Mazembe (DR Congo), Horoya AC (Guinea), Wydad Atheltic Club (Morocco), Simba SC (Tanzania) and Esperance de Tunis (Tunisia) na Al Ahly (Misri).

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.