​Barcelona Watwaa Ubingwa wa La Liga kwa Mara ya Kwanza Tangu 2019

Barcelona

Nyota Robert Lewandowski alifunga mabao mawili na kusaidia Catalans kushinda taji lao kwanza chini ya kocha Xavi Hernandez

Barca watasubiri hadi mechi yao dhidi ya Real Sociedad Jumamosi na Mallorca mnamo 28 Mei kutwaa taji hilo

Barcelona wana pointi 85, 14 zaidi ya wapinzani wao wa karibu Real Madrid


Barcelona wametwaa ubingwa wa taji la ligi ya Uhispania, La Liga kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 2019 siku ya Jumapili, Mei 14, wakipiga Espanyol 4-2.


Wachezaji wa Barcelona wakishehereka ushindi wao Jumapili. Picha: David Ramos. Chanzo: Getty Images

Nyota Robert Lewandowski alifunga mabao mawili na kusaidia Catalans kushinda taji lao kwanza chini ya kocha Xavi Hernandez aliyeteuliwa mnamo Novemba 2021, na la kwanza bila huduma za aliyekuwa mnogeshaji wao Lionel Messi.


Miamba hao walitwaa ushindi huo pia baada ya kuishinda Real Madrid kwenye Kombe la Uhispania la Super Cup mnamo Januari 2023.


Jinsi Barca walishinda taji la La Liga

Barca walikuwa kifua mbele kwa mabao 3-0 hadi muda wa mapumziko, Robert Lewandowski akifunga bao lake la 20 la ligi msimu huu kabla ya Alejandro Balde, 19, kufunga bao la pili.


Lewandowski aliongeza bao la tatu kabla ya Jules Kounde kufunga bao nne kupitia kichwa na kufanya mambo kuwa 4-0.


Espanyol ilijaribu kusawazisha kupitia kwa Javier Puado na Joselu lakini mabao yao yalisalia kuwa ya kuvutia machozi tu.


Barcelona wana pointi 85, 14 zaidi ya wapinzani wao wa karibu Real Madrid, zikiwa zimesalia na pointi 12.


Wakati huo huo, Espanyol wako katika hatari ya kushushwa daraja kwa mara ya pili katika misimu minne kutoka kwa La Liga baada ya kushindwa katika mechi 11 za ligi.Espanyol kwa sasa wana pointi nne kutoka kwa mduara wa hatari zikiwa zimesalia mechi nne.


Barca watasubiri hadi mechi yao dhidi ya Real Sociedad Jumamosi na Mallorca mnamo 28 Mei kutwaa taji hilo.Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.