TIMU ya Wanawake ya JKT Queens imefanikiwa kutetea ubingwa wa Ngao ya Jamii 2025 kwa Wanawake kufuatia ushindi wa 2-1 dhidi ya Simba Queens kwenye fainali katika dimba la KMC Complex.
FT: JKT Queens 2-1 Simba Queens
⚽ 12’ Winfrida Gerald
⚽ 18’ Asha Omary (OG)
⚽ 90+4’ Zawadi Usanase
Kwenye mchezo wa mapema, Yanga Princes iliibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Mashujaa Queens kwenye mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu.