Mzize Abeba Matumaini Yanga Kufuzu Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa CAF




Kama kuna mchezaji ambaye mashabiki wa Yanga wanatamani kumuona uwanjani siku ya Jumamosi katika mchezo dhidi ya Silver Strikers, basi ni Clement Mzize


Mzize anaonekana kama tumaini la Yanga katika eneo la ushambuliaji hasa baada ya washambuliaji tegemeo Prince Dube na Andy Boyeli kusuasua katika mechi iliyopita

Mzize hakucheza Malawi licha ya kuwa tayari alikuwa amepona majeraha yaliyomuwa nje kwa takribani wiki tatu

Benchi la ufundi walichukua uamuzi wa kumpumzisha ili kuhakikisha anaimarika kwa asilimia 100


Mshambuliaji huyo ambaye Yanga ililazimika 'kuvunja benki' kumbakisha katika dirisha lililopita la usajili, sasa anabeba matumaini ya Wananchi kuelekea mchezo wa Jumamosi ambao Yanga inahitaji ushindi wa kuanzia mabao mawili ili kutinga hatua ya makundi

Habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni kuwa mpaka sasa wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huo, hakuna mchezaji majeruhi

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad