Huyu Simba Walimwona Hafai, Yanga Kaenda Kageuka Kuwa Lulu




ISRAEL PATRICK MWENDA, Wakati anajiunga na mitaa ya Twiga na Jangwani wengi hawakuona kama anaweza kwenda kuingia moja kwa moja kikosini, kuanzia Msimbazi hadi Young Africans kote watu walidhani atakaa zaidi nje ya uwanja kuliko ndani lakini mambo yamekuwa tofauti

Mitaa ya Twiga na Jangwani iliamua kumpa mkataba kijana huyu kisha yeye akawapa imani ya kiwango bora uwanjani tangu msimu jana, hadi sasa ni miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha kwanza pale, msimu huu umeanza na ameendeleza alichomaliza nacho msimu uliopita chini ya Miloud Hamdi

Upande wa beki wa kulia hati miliki imekuwa yake na timu nzima imani ipo kwenye ubongo na miguu yake, ni eneo lile ambalo wapo Kibwana Shomari pamoja na Yao Kouassi mwenye majeraha bado ambao wanapaswa kuja kwa utofauti sana ili kupata nafasi mbele ya Israel Patrick Mwenda huyu wa sasa

Uhamisho huu nafikiri wanafurahia sana sababu ni miongoni mwa maeneo ambayo kipindi wanafanya usajili wake uhakika haukuwa mkubwa sana, watu waliona kama ni eneo ambalo halitoshi bado nguvu inahitaji lakini kijana ameingia kikosini na kufanya kazi nzuri iliyojibu maswali mengi ya nje

Simply, huyo tunayemuona sasa ndio yule kijana wa Alliance, KMC hadi Singida Black Stars, mitaa imekubali kuhusu ubora wake na sasa hawana shaka juu yake, One of the best Right-Back 🫡

Anaandika @cheyolutenganotz

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad