TFF Yatangaza Viingilio Ngao ya Jamii Simba vs Yanga

 

TFF Yatangaza Viingilio Ngao ya Jamii Simba vs Yanga

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa Ngao ya Jamii utakaowakutanisha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga SC, dhidi ya watani wao wa jadi, Simba SC, Septemba 16, 2025 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 11:00 jioni.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF leo Septemba 14, 2025, kiingilio cha chini kabisa kwenye mzunguko ni Tsh 5,000/=, huku daraja la VIP C likiwa Tsh 20,000/=, VIP B Tsh 30,000/=, na VIP A Tsh 100,000/=.


Aidha, tiketi za juu zaidi katika daraja la Platinum zitauzwa kwa Tsh 300,000/=.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad