Taifa Stars Kibaruani Leo Dhidi ya Congo Kusaka Ticket Kufuzu Kombe la Dunia




Michuano ya kuwania kufuzu kombe la Dunia la FIFA 2026 kwa ukanda wa Afrika inaendelea tena leo Septemba 05, 2025 ambapo Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itatupa karata yake nyingine kwenye mchezo wa Kundi E dhidi ya Congo Brazaville.

Baada ya mchezo huo utakaopigwa katika dimba la Alphonse Massamba-Debat mjini Brazzaville majira ya Saa moja kamili usiku (1:00) kwa Saa za Afrika mashariki, Stars itacheza tena mchezo mwingine wa kufuzu Kombe la Dunia Septemba 09 dhidi ya Niger katika Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.

19:00 Congo 🇨🇬 vs 🇹🇿 Tanzania

22:00 Morocco 🇲🇦 vs 🇳🇪 Niger

MSIMAMO KUNDI E

1.🇲🇦 Morocco — mechi 5 — pointi 15

2.🇹🇿 Tanzania — mechi 5 — pointi 9

3.🇿🇲 Zambia — mechi 5 — pointi 6

4.🇳🇪 Niger — mechi 4 — pointi 6

5. 🇨🇬 Congo — mechi 5 — pointi 0

7. 🇪🇷 Eritrea — mechi 0 — pointi 0


NB: Eritrea ilijiondoa kwenye michuano hiyo kuepuka wachezaji kutumia fursa ya mechi za nje ya nchi na kutoroka Nchi hiyo kutokana utawala dhalimu wa Rais wa Nchi hiyo, Isaias Afwerki, ambao unalazimisha utumishi wa kijeshi wa maisha kwa watumishi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad