Klabu ya Simbasc bado inaendelea kusaka mlinzi wa kushoto mwenye daraja la Mohamed Hussen ambaye atakuja kuziba nafasi hiyo
Mpaka sasa Simbasc tayari imepokea walinzi wawili wa kushoto ambao wanaendelea kuwafanyia majaribio kama wanaweza kukidhi mahitaji ambayo wanayahitaji
Tayari kwenye kambi yao nchini Misri yupo mlinzi wa kushoto kutoka Cameroon Jonathan Ngwem ambaye ni mchezaji huru kutoka kwenye kikosi cha Feature Fc ya nchini Misri
Pia Simbasc wamempokea mlinzi wa kushoto Hernest Briyock Malonga kwa maangalizi zaidi kama atawafaa
Itoshe kusema namba 3 kwenye kikosi cha Simbasc ni kizungumkuti mpaka sasa viongozi wanaumiza kichwa kumpata mbadala sahihi
Hii ni kutokana na pressure kubwa ambayo iko njee, kwani wakichukua bora mchezaji watu watahoji kwanini walikubali kumuachia Mohamed Husseni kama awana uwakika wa kumpata mbadala sahihi.