Timu ya taifa ya soka ya wanawake, Twiga Stars 🇹🇿 leo inahitaji USHINDI wa pointi tatu dhidi ya Ghana ili kufuzu ROBO fainali ya Fainali ya Mataifa ya Afrika (WAFCON) yanayoendelea Morocco.
Mechi hiyo ya mwisho ya Kundi C itapigwa kwenye Uwanja wa Manispaa ya Berkane na Tanzania inahitaji ushindi tu ili ifuzu na kuandika historia ya michuano hiyo.
Msimamo wa kundi hadi sasa uko wazi Afrika Kusini iliyoko kileleni kwa pointi nne sawa na Mali zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa, huku Tanzania na Ghana zikiwa na pointi moja kila timu.
Twiga ikishinda mechi dhidi ya Ghana, itafikisha pointi nne na kusikilizia ma- tokeo ya mwisho ya Afrika Kusini na Mali ili angalau iangukie katika mshindwa bora (Best Loser)
Kocha wa Stars, Bakari Shime amefunguka kuwa: “Ni kama fainali kwetu, lazima tushinde dhidi ya Ghana tupate alama nne, maandalizi yameenda sawa imani tutshinda.”