Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imetoka nyuma 1-0 na kushinda 2-1 dhidi ya Senegal kwenye mashindano ya CECAFA ya Mataifa matatu katika dimba la Black Rhinos, Karatu Tanzania.
Huu ni ushindi wa pili kwa Stars baada ya kuilaza Uganda The Cranes 1-0 kwenye mchezo wa kwanza wa mashindano hayo ambayo ni sehemu ya maandalizi ya michuano ya CHAN 2024 inayotarajiwa kuanza Agosti 2, 2025.
FT: Tanzania 🇹🇿 2-1 🇸🇳 Senegal
⚽ 53’ Sopu (P)
⚽ 56’ Bacca
⚽ 08’ Mbodji