Real Madrid wako tayari kutoa pauni milioni 100 kwa kiungo wa Manchester City na Hispania Rodri, 29 (Sun).
Winga wa Manchester City na England Jack Grealish, 29, ni mmoja wa wachezaji kadhaa wa upande wa kushoto wanaofuatiliwa na Napoli (Corriere dello Sport).
Javi Guerra amekataa ofa ya kurefusha mkataba wake na Valencia, huku Manchester United ikiripotiwa kumfuatilia kiungo huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 22 (Marca).
Tottenham wanamfuatilia kwa karibu Kobbie Mainoo, huku kiungo huyo wa Manchester United bado hajafikia makubaliano ya kurefusha mkataba wake wa muda mrefu, ambao unamalizika mwaka 2027 (tbrfootball.com).
West Ham watashindana na Everton katika mbio za kumsajili Douglas Luiz kutoka Juventus baada ya Aston Villa kujiondoa kwenye mbio za kumsajili tena kiungo huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 (Sun).
Atalanta wanapanga kumsajili winga wa Liverpool na Italia Federico Chiesa, 27, iwapo Juventus watatoa pauni milioni 43 kumsajili mshambuliaji wa Nigeria Ademola Lookman, 27 (Football Italia).
West Ham wako kwenye mazungumzo na Callum Wilson kuhusu uhamisho huru kufuatia kutemwa kwa mshambuliaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 33 na Newcastle.
Spurs wanafuatilia hali ya mkataba wa Joao Palhinha wa Bayern Munich. Klabu hiyo ya Bavaria iko tayari kufanya mazungumzo iwapo ofa itapelekwa kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 30 (Florian Plettenberg).
RB Leipzig wamemtaja kiungo mshambuliaji Xavi Simons katika kikosi chao cha kambi ya mazoezi, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kuhusishwa na uhamisho kwenda Chelsea ambapo mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi ameshafanya mazungumzo kuhusu masharti binafsi na The Blues (Standard).
Manchester City wanataka kumshikilia Ederson licha ya Galatasaray kuonyesha nia kwa kipa huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 31, ambaye anakaribia kuingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake (The Independent).
Borussia Dortmund wanavutiwa na mpango wa kumsajili kiungo wa Brighton Facundo Buonanotte, 20. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina alitumia msimu uliopita kwa mkopo Leicester City na ana miaka mitatu iliyobaki kwenye mkataba wake (Sky Sports).
Mazungumzo kati ya Marseille na Feyenoord kwa ajili ya winga wa Brazil Igor Paixao yamekwama baada ya ofa ya pauni milioni 24 ya klabu ya Ufaransa kutofikia bei inayohitajika (RMC).
Leeds United sasa wana matumaini ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 (Yorkshire Evening Post).
Kiungo wa Uturuki Hakan Calhanoglu amehusishwa na uhamisho kutoka Inter Milan lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anasema anataka kubaki kwenye klabu hiyo ya Italia (Gazzetta dello Sport).