Afisa habari wa klabu ya Yanga Sc Ali Kamwe ametuma ujumbe mzito kwa viongozi na mashabiki wa klabu ya Simba Sc kuhusiana na tetesi zinazoeleza kwamba viongozi wa klabu hiyo tayari wamefanikiwa kuinasa saini ya Jonathan Sowah.
Vyanzo mbalimbali vya habari za michezo nchini Tanzania vimedokeza kwamba Simba Sc wamefanikiwa kuinasa saini ya Jonathan Sowah kwa mkatana wa miaka miwili na muda wowote kuanzia sasa nyota huyo anaweza kutambulishwa kama nyota mpya wa miamba hiyo ya soka la Tanzania bara.
Mara baada ya tetesi hizo kushika kasi kwenye mitandao ya kijamii, Ali Kamwe ameibuka na taarifa nzito ambayo inalenga kuwakejeli Simba Sc kwa kukamilisha dili la Jonathan Sowah kutoka katika klabu ya Singida Black Stars.
Ali Kamwe kupitia ukurasa wake wa Instagram amechapisha taarifa nzito inayoeleza kwamba yeye kama Baba mdogo wa Jonathan Sowah amefurahi sana mara baada ya kuona mtoto wake huyo amefanikiwa kupata timu mpya.
Ikumbukwe kwamba Jonathan Sowah aliwai kusema kwamba anamuona Hersi Said kama Baba mlezi kwake kwani alimtoa kwenye mazingira magumu na akamsaidia kumleta katika klabu ya Singida Black Stars.
Sowah na Hersi Said ni watu wanaotajwa kuwa na mahusiano ya karibu sana na hapo ndipo anaibukua Ali Kamwe kwa kueleza kwamba yeye ni Baba mdogo wa Sowah kwa sababu yeye ni bosi huyo wanafanya kazi katika taasisi moja na kuna wakati huwa wanaishi kama mtu na kaka yake.
Je, wewe kama mdau mkubwa wa soka la Tanzania bara unatoa maoni gani kuhusiana na taarifa hii iliyotolewa na Alikamwe kuhusiana na uhamisho wa Sowah kwenda Simba Sc?.