Mshambuliaji wa Brentford Yoane Wissa angependelea kumfuata meneja wa zamani wa Bees Thomas Frank kwenda Tottenham, licha ya Newcastle United kuonyesha nia ya kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), 28. (Talksport)
Everton wamewasilisha ombi la kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz kutoka Juventus, huku Aston Villa na West Ham pia zikimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (TeamTalk)
Arsenal wanakaribia kukamilisha mkataba wa kumsajili mshambuliaji wa Uswidi Viktor Gyokeres kutoka Sporting, huku The Gunners wakimgfania uchunguzi wa kimatibabu wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Football Transfers)
Arsenal walimnunua kiungo wa kati wa Ureno Joao Palhinha, 30, mapema msimu huu lakini hawakuweza kuafikiana na Bayern Munich. (Bild - in Germany)
Nottingham Forest wanafanya juhudi kubwa kumshawishi kiungo wa kati wa Uingereza Morgan Gibbs-White, 25, kukabidhi mustakabali wake wa muda mrefu katika klabu hiyo huku kukiwa na nia ya kuongezeka kutoka kwa Tottenham. (Givemesport)
Inter Milan wamependekeza mpango wa kumchukua mshambuliaji wa Nigeria Ademola Lookman kwa mkopo na ada ya £34.6m kumnunua lakini Atalanta hawana nia ya masharti hayo na wanataka £43.2m kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Sky Sports Italia - in Italian)
Leeds United wapo kwenye mazungumzo juu ya kumsajili winga wa Feyenoord Mbrazil Igor Paixao, 25. (Sky Sports)
Luton Town wanatazamiwa kusaini mkataba na kipa wa Jamhuri ya Ireland Josh Keeley kutoka Tottenham baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kushindwa kuafikiana kandarasi mpya na Spurs. (Standard)
West Ham wako kwenye mazungumzo ya kumleta mlinzi wa Uingereza Kyle Walker-Peters, 28, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Southampton na amejiondoa katika uhamisho wa kwenda Besiktas. (Givemesport)
Arsenal wamekubali ada ya takriban pauni 200,000 ya Salford City kumnunua mshambuliaji wa Uingereza Will Wright katika juhudi za kuipiku Liverpool kwenye usajili. (Mail)
Mshambulizi wa Brighton na Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 20, yuko kwenye mazungumzo ya kujiunga na Roma msimu huu wa joto. (Fabrizio Romano)