Simba SC Wampa Mkono wa Kwaheri Valentin Nouma

Simba SC Wampa Mkono wa Kwaheri Valentin Nouma
Valentin Nouma


Beki wa kushoto raia wa Burkina Faso, Valentin Nouma, ameaga rasmi klabu ya Simba SC baada ya kufikia makubaliano ya pande zote kuhusu kusitisha mkataba wake.

Kupitia kurasa zake za Instagram na Facebook, Nouma ameandika ujumbe wa kuagana na mashabiki wa Simba akisema:

"Kwa makubaliano ya pamoja, safari yangu na Simba SC inafikia mwisho. Ushindani ukiwa ndio lengo langu kuu, ninapitia mapendekezo mbalimbali, na mara tu uamuzi utakapokuwa rasmi, nitachapisha kuhusu safari yangu mpya. Shukrani kwa familia nzima ya Simba na wote waliokuwa wakinipa nguvu ya kusonga mbele — ilikuwa ni safari nzuri sana.

NguvuMoja"

Kuondoka kwake kunaongeza orodha ya mabadiliko yanayoendelea kwenye kikosi cha Simba kuelekea msimu wa 2025/2026.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad