Mobile

Saleh Jembe; Kipi cha Ajabu? Zimbwe Ana Haki ya Kutafuta Maslahi

 

Saleh Jembe; Kipi cha Ajabu? Zimbwe Ana Haki ya Kutafuta Maslahi

Mwandishi mkongwe na maarufu wa michezo nchini, Saleh Ally maarufu kama Saleh Jembe

Mwandishi mkongwe na maarufu wa michezo nchini, Saleh Ally maarufu kama Saleh Jembe, amefunguka kuhusu uhamisho wa beki wa zamani wa Simba SC, Zimbwe Jr, kuelekea kwa watani wao wa jadi Yanga SC.


Kupitia andiko lake lenye tafakuri ya kipekee, Saleh ameandika:


“Kipi cha ajabu? Zimbwe Jr hawezi kuwa mchezaji wa kwanza kuhama Simba kwenda Yanga, wala wa kwanza kuihama Simba.”


Saleh anasema licha ya mashabiki wengi wa Simba kujawa na hisia kali na maneno kama “Kaniumiza sana, Imeniuma sana,” bado ni muhimu kutazama upande wa pili wa maisha ya mchezaji.


“Si jambo baya kishabiki, lakini kuna mengi ya kufikiria na kubungua bongo. Maisha ya mchezaji ni muhimu zaidi. Kama Zimbwe ametumikia Simba kwa zaidi ya misimu 11, hakuna anachodaiwa. Wampongeze tu,” ameandika Saleh.



Mohamed Hussein Zimbwe Jr

Zimbwe Jr amecheza robo fainali na fainali nyingi za Ligi ya Mabingwa Afrika, fainali ya Kombe la Shirikisho CAF, na amefanikisha kutwaa makombe yote ya ndani akiwa na Wekundu wa Msimbazi.


Kwa Saleh, mchezaji huyo hana jipya atakalokosa, lakini anasema:


“Umri unaenda. Kama kuna maslahi zaidi, hana ujanja. Ana familia, na anakwenda mwishoni. Hili ni suala la kawaida kwa mchezaji aliyekaa kwa muda mrefu kwenye klabu moja.”


Akiendelea, Saleh Jembe anawaasa mashabiki kutafakari:


“Jiulize: Baada ya misimu 11 ya ligi akiwa Simba (na angalau msimu mmoja Kagera), bado Zimbwe ni mali sokoni, na amesajiliwa kwa dau kubwa. Kuna ubaya upi? Hii ni sifa kwa Simba waliomtengeneza mchezaji wa kiwango hicho.”


Kwa Saleh, ni fahari kwa Simba kuwa na beki aliyewatumikia kwa zaidi ya muongo mmoja na bado anahitajika na klabu nyingine kubwa.


“Simba hawana cha kulalamika. Badala yake, wampongeze na kumtakia heri. Ni nahodha msaidizi ambaye alihudumu MVUA na JUA, na sasa anakwenda mahali pengine kama mchezaji mpya.”


Mwandishi huyo maarufu anahitimisha kwa kusema kuwa maisha ya mpira hayakamiliki bila mshikamano wa pande zote: wachezaji, makocha, viongozi na mashabiki.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad