Inaelezwa kuwa kiungo mshambuliaji wa Simba SC raia wa Ivory Coast, Jean Charles Ahoua kwenye rada za Klabu ya JS Kabylie ya nchini Algeria kwa ajili ya msimu ujao wa 2025/26.
Kwa mujibu wa chanzo cha Habari kutoka ndani ya Simba SC kilieleza kuwa mazungumzo yanakwenda vizuri kati ya uongozi wa Simba na JS Kabylie katika kukamilisha dili hilo la usajili.
Ahoua ni namba moja kwa utupiaji ndani ya ligi alifunga jumla ya magoli 19 na kutoa pasi 9 za magoli akiwa na uzi wa Simba SC msimu wa 2024/25.
Ikiwa dili litajibu Ahoua anatarajiwa kuwa mchezaji wa pili kutoka katika Ligi Kuu Tanzania Bara kujiunga na JS Kabylie, mwingine ni kiungo mchezeshaji, Arthur Bada aliyejiunga na kikosi hicho akitokea Singida Black Stars.