KISA KUSUASUA KWA USAJILI.
Tetesi zinadai kwamba kocha mkuu wa wekundu wa Msimbazi 'Fadlu Davies' amehitaji kikao kazi na viongozi wa klabu ili kufanya tathmini ya haraka kuhusu muelekeo wa klabu kunako dirisha hili la usajili na hatma yake ndani ya klabu hiyo,
IKUMBUKWE:
Kwamba tayari kocha huyo alishafanya mazungumzo ya awali na klabu za kutokea kwao Afrika kusini na mezani ana ofa kadhaa kutokea vilabu vy kaskazini mwa jangwa la Sahara (Uarabuni),
Hivyo kocha ameuarifu uongozi kuwa endapo hatotimiziwa mahitaji yake ya kupatiwa wachezaji anaowahitaji kuelekea msimu ujao, basi haitokuwa sehemu ya kikosi hicho muda wowote kabla ya kuanza kwa preseason.
Bundi ameanza kuzurula mitaa ile.