Mobile

Kisa Mshahara Kocha ASEC Mimosas Aipiga Chini Offer ya Yanga....

Kisa Mshahara Kocha ASEC Mimosas Aipiga Chini Offer ya Yanga....


Kocha wa klabu ya ASEC Mimosas, Julien Chevalier, amekataa kujiunga na Yanga SC baada ya pande hizo mbili kushindwa kufikia makubaliano ya maslahi.

Kwa mujibu wa kocha huyo ameeleza kuwa alikuwa na ofa ya klabu ya Tanzania lakini wameshindwana kulingana na kushindwa kufikia katika suala zima la maslahi binafsi. Yanga ilimpa kocha huyo ofa ya mshahara wa takriban milioni 28 kwa mwezi, lakini Chevalier alitaka alipwe milioni 40 kwa mwezi kiasi ambacho uongozi wa Yanga umeshindwa.

Kutokana na hali hiyo, Yanga sasa imeelekeza macho yake kwa makocha wengine ili kujaza nafasi hiyo muhimu. Hii si mara ya kwanza kwa Yanga kushindwa kufikia makubaliano na kocha mkubwa; hivi karibuni pia walishindwa kumvutia Rulani Mokwena, aliyekuwa kocha wa Wydad, ambaye sasa amejiunga na MC Alger ya Algeria.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad