Huu Hapa Ukweli Wote Kuhusu Manula Kwenda Azam Kirahisi

 

Huu Hapa Ukweli Wote Kuhusu Manula Kwenda Azam Kirahisi

HUKU ikitaja sababu tatu za kumrejesha golikipa, Aishi Manula kundini baada ya kumpoteza kwa kipindi cha miaka minane, uongozi wa Azam FC, umesema ujio wa Aishi Manula katika klabu hiyo ni pendekezo la Kocha Mkuu Florent Ibenge.

Klabu hiyo ilimtangaza rasmi kuwa mchezaji wao juzi, ingawa  hili lilianza kufahamika kuwakipa huyo kutimkia Azam tangu Juni 11, mwaka huu.

Manula alijiunga na Simba mwaka 2017, akiwa na wachezaji wenzake, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni na John Bocco, ambapo kati ya hao wote ni Kapombe tu ambaye amesalia.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Jana, Ofisa Habari wa Klabu hiyo Thabit Zakaria maarufu Zaka Zakazi, alisema Kocha huyo alimpendekeza mlinda mlango huyo kutokana na kutambua thamani yake.

“Tusingeweza kumsajili Manula bila kuzungumza na kocha, ameridhia ndio maana tukamjumuisha kwenye kikosi chetu,” alisema Zaka Zakazi.


Alisema Manula ni miongoni mwa wachezaji wazuri, hivyo anaamini ataleta mafanikio makubwa msimu ujao kutokana na ubora wake.

Mbali na Manula pia Himid Mau amerejea katika klabu hiyo ili kuipa nguvu timu yao kuelekea msimu ujao.

Alipoulizwa Zaka Zakazi, juu ya usajili huo, alisema hawezi kuzungumzia usajili huo mpaka hapo utakapokamilika.

Manula amejiunga na Azam FC kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Simba.

Aidha, Zaka Zakazi alisema, mbali na Ibenge, kingine kilichosababisha Manula kurejeshwa kundini baada ya kuwa nje kwa miaka minane ni upatikanaji wake kutokuwa mgumu kwani alikuwa amemaliza mkataba wa Klabu ya Simba.

Kingine ni umaarufu na ubora wake, pia ni kijana wao wa nyumbani, hivyo ni vitu ambavyo vimesababisha wasisite kumrejesha kwenye viunga vya Chamazi.

“Tumeangalia vitu vingi mpaka tumeamua kumrejesha, kwanza upatikanaji wake, ubora wake, ni kipa anayejulikana nchini, pia ni kijana wetu, anarudi nyumbani, kila mmoja alikuwa amemmisi mwenzake.

“Limekuwa ni jambo la heri kwamba tumefanikiwa kumrudisha kijana wetu nyumbani sasa tuendelee na maisha. Tumempa mkataba wa miaka mitatu kwa hiyo yupo hadi 2028,” alisema

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad